KUWATUMIA WATOTO KINGONO NI KOSA LA JINAI.
KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KIFUNGU 138B.
Kifungu tajwa hapo juu kinasema;
138B.-(1) Mtu yeyote ambaye-
(a) akiwa anafahamu anamruhusu mtoto yeyote kuwa kwenye sehemu yoyote kwa nia ya kumsababisha mtoto kudhalilishwa kijinsia au kushiriki kwa namna yoyote katika matendo ya ngono au maonyesho ya ngono;
(b) anajifanya kuwa ni kuwadi wa mtoto kwa nia ya kufanya ngono au namna yoyote ya udhalilishaji kwa ngono, au maonyesho ya ngono;
(c) anamlaghai mtu kuwa yeye ni mteja wa mtoto kwa nia ya ngono au aina yeyote ya udhalilishaji wa kijinsia, au maonyesho ya ngono, kwa njia ya matangazo au kwa kutumia vyombo vya habari, matangazo kwa njia ya mdomo au namna nyingine zinazofanana na hizo;
(d) anatumia vibaya uwezo wake au mahusiano yake aliyonayo kwa mtoto, akamlaghai mtoto kufanya matendo ya ngono au namna yoyote ya udhalilishaji wa kijinsia au maonyesho ya kudhalilisha ya ngono;
(e) anamtishia, au akitumia nguvu kwa mtoto, kwa nia ya kumlazimisha mtoto kufanya ngono au kwa namna yoyote ya kumdhalilisha mtoto kwa ngono au maonyesho ya ngono;
(f) anampa mtoto au wazazi wake fedha, vitu au mafao mengine kwa nia ya kumkuwadia mtoto huyo afanye ngono au namna yoyote ya udhalilishaji wa ngono au maonyesho ya ngono,
Atatenda kosa la kumtumia mtoto kwenye matendo ya ngono na atawajibika kwa adhabu ya kifungo kisichopungua miaka kumi na mitano jela na kisichozidi miaka thelathini.
Imeandikwa na @yesayajm_
Jungu la sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿