Kwa MUJIBU wa sheria ya makampuni na kanuni kuhusu wamiliki manufaa wa kampuni, kila kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria ya makampuni inatakiwa kuwasilisha kwa msajili wa makampuni, taarifa zote kuhusu wamiliki manufaa wa kampuni kwa lengo la kudhibiti utakatishaji fedha, rushwa na ugaidi. Wamiliki manufaa ni watu wenye uwekezaji mkubwa kabisa katika kampuni, au wenye kubeba dhamana ya mwisho ya uendeshaji wa kampuni hata kama hawapo katika nyaraka za kampuni.
#sherianatehama
#sheria

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿