Kwa MUJIBU wa sheria ya ardhi na sheria ya uwekezaji, pamoja na kuwa watu ambao sio watanzania hawaruhusiwi KUMILIKI ardhi ya Tanzania, lakini sheria hizo zimeweka mianya ambapo wageni wanaweza kutumia ardhi ya Tanzania. Wageni wanaweza kupewa ardhi kupitia kituo cha uwekezaji kwaajili ya shughuli za kibiashara tu, wageni wanaweza kuingia MIKATABA ya kutumia ardhi ya Tanzania ambayo inamilikiwa na raia wa tanzania, mwisho wageni wanaweza kufungua kampuni Tanzania yenye asilimia 51% ya wanahisa ambao ni watanzania hivyo kampuni hiyo kuwa kampuni ya kitanzania yenye haki ya KUMILIKI ardhi.
#sherianatehama
#sheria

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿