Ticker

6/recent/ticker-posts

Kujaribu kujiua na kinga yake kisheria.

 


Kwa mujibu wa kifungu cha 217 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, kujaribu kujiua ni kosa la jinai. Kosa hilo linaweza kuhukumiwa kwa adhabu isiyozidi miaka 5 jela kama inavyoelekezwa na kifungu cha 35 kinachoeleza adhabu ya jumla kwa makosa ambayo hayajapewa adhabu ya moja kwa moja.

Lakini sheria hiyohiyo inaweka kinga katika kifungu cha 13 na inatoa msamaha kwa watu wanaofanya makosa wakiwa katika hali ya ugonjwa unaoathiri akili zao na kufanya wasielewe wanachofanya.

Hivyo basi, endapo mtu amejaribu kujiua akiwa na akili timamu na ikathibitika hivyo, atahukumiwa kwa adhabu isiyozidi miaka 5, lakini kama amejaribu kujiua akiwa na hali ya ugonjwa unaoathiri akili yake na kufanya kosa bila kuelewa, hatakuwa na kosa kisheria kwa kuwa sheria inampa kinga.

Endapo mtu huyo amefikishwa mahakamani, na ikabainika alifanya kosa akiwa katika hali ya ugonjwa, Basi mtu huyo hana hatia, mahakama inaweza kuamua mtu huyo kupelekwa katika kituo cha uangalizi wa watu wenye changamoto ya afya ya akili kwa mujibu wa kifungu cha 219(2)(b) Cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura namba 20.

Chapisha Maoni

0 Maoni